Visa vya mimba za utotoni vimeendelea kuongezeka mjini Malindi, Kaunti ya Kilifi, hali iliyowafanya wakazi kuitaka serikali, wazazi na walimu kuongeza juhudi za kuwaelimisha watoto kuhusu madhara ya mimba za mapema.

Amani Charo ambaye ni mzazi amesema umaskini, matumizi mabaya ya teknolojia na utovu wa nidhamu ni baadhi ya sababu zinazochangia tatizo hilo.

AdvertisementIn-article placement — advertise with Kilele Radio

Naye Francis Kalama amesema baadhi ya watuhumiwa wa kuwapa mimba watoto wa chini ya miaka 18 hukwepa mkono wa sheria kupitia hongo, akitoa wito kwa serikali kuchukua hatua kali kukomesha hali hiyo.