By:Robert Wafula Mutasi

Daktari mmoja nchini Kenya amewasilisha ombi bungeni akitaka tatizo la kudumu la ukosefu wa nguvu za kiume litambuliwe rasmi kama ulemavu.
AdvertisementIn-article placement — advertise with Kilele Radio
Daktari Benson Kibore amesema vijana na watu wa umri wa makamo ndio wanaoathirika zaidi na tatizo hilo, akisisitiza kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza unyanyapaa na kuboresha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa waathiriwa.