By:Hassan Pojjo

Mkufunzi wa timu ya Chaani Youth, Jones Kyalo, maarufu kama Viera, amewataka wazazi kuhakikisha watoto wao wanajiandaa kwa mechi za kirafiki zitakazochezwa Jumapili hii.

AdvertisementIn-article placement — advertise with Kilele Radio

Kocha huyo amesema wachezaji wa makundi ya umri wa chini ya miaka 9, 11 na 14 watamenyana na wenzao wa Regional Soccer Academy katika mechi zitakazofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi ya Mvita kuanzia saa nane mchana.

Ameeleza kuwa mechi hizo ni sehemu ya kukuza vipaji, kuwajengea vijana uzoefu wa ushindani na kuwaandaa kwa mashindano yajayo.

Vilevile, Viera amewafahamisha wazazi kuwa msafara wa timu utaondoka Kipevu saa saba mchana kuelekea Mvita, akisisitiza umuhimu wa watoto kufika kwa wakati ili maandalizi yakamilike mapema.