By:Hassan Pojjo

Wanafunzi nchini huenda wakapata afueni ya changamoto za usafiri baada ya shirika moja kuanzisha mpango wa kuleta matatu yanayotumia umeme.
AdvertisementIn-article placement — advertise with Kilele Radio
Mbunge wa Jomvu, Badi Twalib, amesema amefanya kikao na wadau wa shirika hilo kujadili namna ya kutekeleza mpango huo, ambao unalenga kuboresha huduma za usafiri kwa gharama nafuu na rafiki kwa mazingira.
Badi amesema kuwa endapo mpango huo utafanikiwa, wanafunzi watanufaika kwa kupata usafiri salama, wa uhakika na unaotumia teknolojia ya kisasa ya nishati safi.
Ameongeza kuwa ushirikiano kati ya viongozi na sekta binafsi ni muhimu katika kuleta suluhisho la changamoto za usafiri na kuchangia maendeleo ya jamii.