By:Athuman Luchi

Mwavumbo Super Cup imefungua jukwaa muhimu kwa wasichana wa mashinani kuonyesha vipaji vyao katika soka.

AdvertisementIn-article placement — advertise with Kilele Radio
VOICED PACKAGE

Mashindano hayo yanayoongozwa na Dzame Fatuma yamewashirikisha timu sita za wasichana kutoka Village Unit ya Kalalani, yakilenga kuibua vipaji vipya na kuwapa vijana fursa sawa katika michezo.

Kupitia #LindaUjanaWako na #MentalHealthMatters, mashindano hayo pia yanahamasisha vijana kuhusu afya ya akili na matumizi bora ya muda.

Mwavumbo Super Cup inalenga kujenga njia ya vipaji vya mashinani kufikia viwango vya kitaifa na kimataifa.