By:Hassan Pojjo

Mashindano ya Kamoti Junior Super Cup makala ya tatu yataendelea Jumamosi, Agosti 1, 2026, huku timu nne zikitarajiwa kushuka dimbani katika mechi mbili za kusisimua zitakazofanyika katika Kaunti ya Kilifi.
Katika Uwanja wa Mgala, Red Scorpion FC itachuana na Young Strikers FC kuanzia saa 9:00 alasiri, huku kila timu ikisaka ushindi muhimu wa kusonga mbele kwenye mashindano hayo.
Wakati huohuo, katika Uwanja wa Lugwe, Lexcon FC itamenyana na M’Barakani FC, pia kuanzia saa 9:00 alasiri, katika pambano linalotarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na ubora wa vikosi vya timu hizo.
Waandalizi wamesema maandalizi yote yamekamilika ili kuhakikisha michezo inafanyika katika mazingira salama na yanayozingatia kanuni za mashindano. Vilevile, wamewahimiza mashabiki kujitokeza kwa wingi kuzipa sapoti timu zao huku wakidumisha amani na nidhamu viwanjani.
Kamoti Junior Super Cup imeendelea kujidhihirisha kama jukwaa muhimu la kuibua vipaji vya wachezaji chipukizi katika ukanda wa Pwani, huku ikitoa fursa kwa vijana kuonekana na makocha, viongozi wa vilabu na wadau wa soka.
Mashabiki wanatarajiwa kushuhudia michezo yenye ushindani, kasi na ufundi wa hali ya juu huku kila timu ikipigania nafasi ya kusonga mbele kuelekea ubingwa wa Kamoti Junior Super Cup makala ya tatu.