
Nafasi ya Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini, IEBC, imetangazwa rasmi huku Wakenya wenye sifa wakialikwa kutuma maombi.
Kwa mujibu wa taarifa ya IEBC, atakayeteuliwa pia atahudumu kama Katibu wa Tume na Afisa Mkuu wa Uhasibu, akisimamia utekelezaji wa sera za tume pamoja na shughuli zake za kila siku.
AdvertisementIn-article placement — advertise with Kilele Radio
Nafasi hiyo imekuwa wazi tangu aliyekuwa Katibu na Afisa Mkuu Mtendaji, Marjan Hussein Marjan, aondoke mapema mwaka huu.
Kwa sasa, Moses Ledama Sunkuli anaendelea kuhudumu kwa muda akisubiri uteuzi wa afisa mkuu mpya wa kudumu.